MAKALA MAALUM: Wanafunzi wanaokamia masomo hatarini kupoteza kumbukumbu (2024)

Miguu iliyoingizwa kwenye bakuli lenye maji.

WATAALAMU bingwa na bobezi wa magonjwa, afya ya akili na mfumo wa fahamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, wameeleza namna ubongo unavyoathiriwa kutokana na maradhi na kusababisha mtu kupoteza kumbukumbu.

Mbali na tafsiri hiyo hasi kwa ubongo, pia wanaeleza uwezo wa kiungo hicho muhimu na injini ya mwili kilivyo na utaratibu maalum wa kupoteza kumbukumbu mbaya, ikiwa ni matokeo chanya kuulinda ubongo.

Pia wanaonya jamii, hasa wanafunzi kutoyakamia masomo, hususan msimu wa mitihani, wakisema ubongo unapotwishwa mzigo mkubwa, hushindwa kutenganisha kumbukumbu ipi itumike sasa na ipi baadaye na kuwasababishia kupata matokeo hasi.

Kwa nyakati tofauti katika mjadala uliopewa jina la ‘Uhusiano Kati ya Kupoteza Kumbukumbu na Afya ya Akili’, mabingwa hao wameuelezea ubongo kwa undani namna unavyotenda kazi.

Bingwa Mbobezi wa Afya ya Akili na Mfumo wa Fahamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk. Damas Mlaki, akiwasilisha mada kuhusu kiungo hicho, anasema taaluma yake inahusika katika kutibu waliopata maradhi na kuathiri ubongo kama vile kiharusi na ajali.

“Huwa ninashughulika na waliopata kiharusi na kupata changamoto ya usikivu na kupoteza kumbukumbu au aliyepata ajali, kisha akapata athari kwenye ubongo na kubadili mwenendo wa kiungo hicho kitabia,” anasema bingwa huyo.

Alisema yumo pia katika kufanya uchunguzi wa kisa chochote ambacho huathiri ubongo, walioumia kichwani na wenye kifafa na kuonesha mabadiliko ya fikra, tabia na mwenendo kulinganishwa na awali.

“Ninaona wazee maana tatizo hili huwakumba zaidi, lakini hata watoto na kundi lingine. Kozi ya taaluma hii niliipata Afrika Kusini, ni wachache wanaofikia hatua hii hasa kwa nchi kama zetu, kwa sababu hadi kuwa bingwa bobezi kuna shahada hata tatu unasomea, zikijikita eneo fulani tu la mwili,” anasema.

KUMBUKUMBU NI NINI?

Bingwa mbobezi huyo katika ubongo anasema kumbukumbu ni kitu kinachohifadhiwa katika ubongo kwa namna mbalimbali, kama vile maneno, picha, sauti, matukio na hata hisia.

“Uwezo ukiwa duni wa kuzipata taarifa ambazo zimehifadhiwa ndio changamoto yaani kama huna uwezo kuzileta, kuhuisha taarifa, ni tatizo tayari katika ubongo.

“Ili utengeneze kumbukumbu lazima milango yako ya fahamu iwe imekamilika, kwa sababu milango mitano ya fahamu ndio lango la kuingilia matukio, hisia, picha, sauti na kuzifanya kuwa kumbukumbu.

Dk. Damas alisema iwapo kumbukumbu itahifadhiwa kama picha, ni lazima macho yawe na uono mzuri, kinyume chake kumbukumbu ya picha kwenye ubongo itaathiriwa.

Pia mlango wa fahamu sikio, anataja kuwa kiungo muhimu cha kupeleka taarifa kwenye ubongo na kuzitunza, na iwapo uwezo wa kusikia ni duni hakuna sauti itakayohifadhiwa.

“Ngozi, kumbukumbu zingine ni za hisia, labda ukigusa lazima ngozi itambue hata bila mguso, hiki ni kitu fulani, kwa hiyo ubongo utatunza taarifa kwa siku nyingine ukiguswa tu ubongo unatumbua ni mazingira fulani,” alisema.

“Kabla hatujasema huyu mtu anapoteza kumbukumbu lazima tuchunguze milango yake ya fahamu ipo sawa? Macho, pua, ngozi, kinywa, masikio.”

Bingwa huyo anazitaja aina ya kumbukumbu; kumbukumbu za matukio (episode memory); kumbukumbu za maarifa (semantic memory); kumbukumbu za ujuzi, utaratibu (procedure memory; kumbukumbu ya hali (condition memory).

Alifanunua kumbukumbu za matukio, anasema inajikita mtu kukumbuka vitu kadhaa kama vile siku ya leo mlo ulikuwa upi, alikwenda wapi, alifika kliniki na kwamba wenye shida katika ubongo huenda wasitambue kama wamekula au la.

“Kumbukumbu ya aina ya pili ni ya maarifa, mfano kukumbuka vitu vya kimaarifa uliyopewa ikiwamo darasani, ukumbuke mji mkuu wa Tanzania ni Dodoma au Uganda ni Kampala, miaka inapita lakini maarifa haya yametunzwa, kinyume chake ni tatizo.

“Aina ya tatu ambayo ni kumbukumbu inayotunzwa na ubongo ni ujuzi. Mfano ukishaelewa namna ya kuendesha gari, au kuandika hutumii tena kumbukumbu. Unaweza kutekeleza bila kufikiri na unaandika vitu vingi bila kufikiri,” alisema Dk. Damas.

Magonjwa yakitokea katika mfumo mmoja huweza kuathiri eneo moja la kumbukumbu, na lingine lisiathirike. Kumbukumbu aina ya nne inahusiana na hali, huzuni, furaha.

“Aina hii iwapo itaathirika taarifa zitaathiriwa mtu hacheki, hana huzuni. Au labda uliwahi kutenda kitu kilikupa furaha sana, ulikutana kimwili na mpenzi wako, ile kumbukumbu haitakutoka na kila unapomuona unakumbuka, unahitaji tena.Msongo wa mawazo baada ya janga ni tatizo, baadhi hushindwa kuchakata kumbukumbu na tukio likiisha huwarudia tena kama vile linatokea sasa.”

Bingwa huyo anataja mbinu za kujikinga na namna ya kufanya ubongo utunze kumbukumbu, kuwa ni kufanya mazoezi ya kimwili na kiakili, lishe bora na kupata usingizi wa kutosha kwa zaidi ya saa nane.

“Kazi kuu ya usingizi ni kurejeaha kumbukumbu. Wanafunzi wanaokesha kusoma bila kuupa nafasi usingizi ni tatizo. Wanaweza hata wanachokisona wasikikumbuke katika chumba cha mtihani. Inahitaji ulale angalau saa nane kwa siku, ili juzihuisha kumbukumbu.

Mbinu nyingine na kutunza kumbukumbu ni kuupa ubongo mazoezi ya kiakili, kuangalia filamu, kusoma vitabu, gazeti, kucheza michezo ya asili kama bao, sababu unatumia fikra ku*mshinda mwenzio mnapocheza. Wazee wanaocheza bao wanarejesha kumbukumbu,” anasema.

UBONGO HUJIKINGA NA ATHARI

Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka hospitali hiyo, Dk. Godwin Mwisomba anasema pamoja na jamii kuwa na dhana wanaopoteza kumbukumbu wanatafsiriwa kwa mtazamo hasi, bado kundi hilo huuponya ubongo.

Anasema kwa ambao wamepitia majanga, matukio ya kutisha maishani, kupoteza kumbukumbu kuhusu matukio hayo husaidia kupunguza mawazo mabaya na athari za kujirudiarudia kwa tukio hilo kwenye akili.

“Upotevu wa kumbukumbu wengi tunapokea kama hasi lakini kwa afya ya akili ni afya. Yaani ni afya mtu kuwa na upotevu wa kumbukumbu fulani.

Akipoteza kumbukumbu kwake ni afya na ni jema husaidia kumwondolea magonjwa yatokanayo na tukio fulani, mfano tukio la maporomoko ya udongo Hanang’, Manyara mtu akishuhudia nyumba, ndugu wanapotea, mtu kama huyu akiipoteza kumbukumbu hii, ni afya.”

Alisema ubongo hujitibu kwa mfumo wake wenyewe, ili kujiweka sawa usiathirike na mfululizo au mlundikano wa matukio mabaya na kusaidia jambo kusahaulika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk. Paul Lawala, anasema jamii hasa familia, iache kufananisha uwezo wa ubongo baina ya mtoto mmoja na nduguze, kwani ni kawaida kutofautiana kutokana na ubongo ulivyoendelezwa.

“Utafiti unafanywa duniani kote, lakini inaonesha uwezo wa ubongo kati ya binadamu mmoja na mwingine hutofautiana, licha ya kuwa na umri sawa hata kama watoto ni wa familia moja. Utakuta mzazi anamsema vibaya mtoto mwenye uwezo mdogo hata kumnyanyapaa. Si sawa!” anaonya.

MAKALA MAALUM:  Wanafunzi wanaokamia masomo hatarini kupoteza kumbukumbu (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Nathanial Hackett

Last Updated:

Views: 6329

Rating: 4.1 / 5 (72 voted)

Reviews: 87% of readers found this page helpful

Author information

Name: Nathanial Hackett

Birthday: 1997-10-09

Address: Apt. 935 264 Abshire Canyon, South Nerissachester, NM 01800

Phone: +9752624861224

Job: Forward Technology Assistant

Hobby: Listening to music, Shopping, Vacation, Baton twirling, Flower arranging, Blacksmithing, Do it yourself

Introduction: My name is Nathanial Hackett, I am a lovely, curious, smiling, lively, thoughtful, courageous, lively person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.